Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

SAFARI YA BAISA KWENYE MZIKI WA INJILI

Hii ni historia Fupi ya muimbaji binafsi wa nyimbo za injili Tanzania anae fahamika kwa jina la BAISA MHELA tafadhari soma mpaka maisho naamini kuna kitu utajifunza kutoka kwa historia hii ya mtumishi huyu wa Mungu kama utamhitaji nitakuwekea mawasiliano yake hapo mwisho wa historia hii.


       Baisa ni muimbaji binafsi wa nyimbo za injiri anae ishi jijini Dar es salaam Tanzania ni mzaliwa wa mkoa wa Morogoro na muumini wa kanisa la BAPTIST, pia ni mhitimu wa mafunzo ya utabibu katika chuo cha Kampala Uniniversity tawi la Dar es salaam hivyo ana taalima ya Udakitari.


                Kipaji chake cha uimbaji wake kiligunduliwa na wazazi,walezi na jamii inayo mzunguka baada ya kuanza kutumika kanisani kwa kuwaongoza watoto wenzake kuimba kwenye kwaya ya watoto wakati huo alikua mtoto mdogo alikua anasoma darasa la awali yani chekechea.


                      Huduma yake ya uimbaji wa kanisani iliendelea mpaka alipofikia umri wa miaka 18 baada ya shirika linalohusiana na vijana la Youth Challange International (YCI) lenye makao makuu yake inchini Canada, shirika hilo lilimchukua kwa lengo la kimtumia kuelimisha katika maswala ya kijamii hapo ndipo aliacha kuimba nyimbo za injili na kuanza kuimba nyimbo za kijamii na nyimbo za kidunia ikiwemo mapenzi.


                     Mnamo mwaka 2013 aliamua kuachana rasimi na mziki wa kidunia na kuanza kuimba nyimbo za injili baada ya wazazi na viongozi wa kanisa walioko mkoani morogoro kumshauri kuachana na mziki wa kidunia, japo alikua ameshapata umaarufu kwenye mziki wa kidunia alitii ushauri wa viongozi hao na kurudi kanisani akatubu ndipo akapewa kibali cha kuhubiri kwa njia ya nyimbo za injili.


                   Kikubwa kinacho mvutia katika uimbaji wake ni neno la Mungu lilivyokua na nguvu na kuwafikia watu wengi na kupokelewa vizuri makanisani pamoja na matamasha mbali mbali ya injili.

   

                    Mafanikio ambayo ameyapata katika uimbaji wake ni kuihubri injili kwa njia ya uimbaji ndani ya nchi ya Tanzania na hata nje ikiwemo nchi jirani ya Kenya, kujiendesha kimaisha pamoja na kuwainua waimbaji chipukizi wa nyimbo za injili ambao hawajiwezi.


                  Mpaka sasa ananyimbo saba za injili ambazo zimesha rekodiwa kwa njia ya Audio nazo ni:

1:USILIE

2:MASIMANGO

3:CHINI YA MSALABA

4:MWAMBIE

5:SIMAMA

6:MFALUME na

7:AMANI

>Katika nyimbo zote saba amefanikiwa kufanya video kwa nyimbo tatu huku akiwa anahitaji maombi yako ili aweze kufanikisha kufanya video kwa nyimbo zote saba, kwa wale mnao hitaji nyimbo hizo zinapatikana kwenye mfumo wa CD,DVD na VCD pia zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii ambayo nitakutajia hapo chini, pia nyimbo zake zinachezwa kwenye vituo tofauti tofauti vya Radio na Televisioni za hapa Tanzania na Kenya.


                Katika nyimbo zote ambazo amesha zirekodi anapenda wimbo wa MWIMBIE MUNGU kuliko nyimbo zote kwasababu ni wimbo ambao alianza kuuimba akiwa mtoto mdogo na alifundishwa wimbo huo na bibi yake MAHUYEMBA ambae amesha tangulia mbele za haki Mungu amlaze mahali pema amen hivyo anapo imba wimbo huo huwa anamkumbuka bibi yake alie kuwa akimpenda sana.

  

>Na huu ndo mwisho wa historia fupi ya muimbaji binafsi wa nyimbo za injili Baisa Mhela kwa maoni au ushauri, kazi na jambo lolote mtafute kwa mawasiliano yafuatayo.

         


 CONTACT:

                >+255 652 155 399

                 >+255 767 671 470

                  >baisamhela@rocketmail.com

               >Facebook.com/BAISA MHELA

               >Instagram.com/BAISA MHELA

               >twiter.com/BAISA MHELA

               >YouTube.com/BAISA MHELA



                  #Mc Goodluck

                         Contact: +255 713 305 650

                  >goodluckmc999@gmail.com

      

       Tangaza na PLAN MEDIA 


Chapisha Maoni

4 Maoni

  1. Nimefurahi sana kukufahamu, zaidi ungetuwekea na track zako tukazipata hapa ingependeza

    JibuFuta
    Majibu
    1. Usijali mtu wa Mungu track zinakujia hivi karibuni kaa mkao wa kula chamsingi endelea kutembelea PlanMedia

      Futa
  2. Mungu akutangulie na kukuinua zaidi Maana Kipaji ulicho nacho ni kikubwa mno Mungu alimuuliza Musa una nini Musa akasema nina fimbo akamwambia Aitumie na kweli aliitumia mpaka ikawafanya wana wa Israel watoke utumwani.... Hata sasa Mungu amekupa hicho kipaji ni Fimbo itumie katika kumuaibisha Shetani pia kumtumikia Mungu na Zaidi itakusaidia hata wewe katika maisha..... Maana Mungu anatupa vipawa ili vimtumikie, viwatumikie watu na Pia vitutumikie sisi yaani kutusaidia katika Maisha yetu.... so My young Brother Baisa go on, keek on pressing on God is going to use you for Nations and you gonna see his blessings.......... so go go go go go!!!!!!!! in the name of Jesus

    JibuFuta