Habari
Tanzania… Habari yako msaka hekima ndani ya Plan Media… Hapa ndipo nyumbani,
nakukaribisha ndugu na jirani ili tushiriki nilichonacho kwa leo, na leo sasa
nina Good News toka kwa Meddy Merchades.
Tuwekane
wazi mpenzi msomaji, hivi unamjuaje huyu Yesu, unaamini nini kuhusu injili?,
kabla hujanijibu nikukutanishe na shuhuda za matendo makuu ya Bwana
aliyomtendea ndugu yetu, km nilivoipokea ndivo ninavoipost hapa
chini>>>
USHUHUDA
Kwa jina naitwa meddy merchades, ni mwanachuo katika chuo cha utumishi wa umma, kwanza uzima
wangu leo ni ushuuda tosha katika maisha langu, naomba nitakutumia ushuuda
wangu. Ilikuwa mwaka 2013 nikiwa form two, mwezi wa tatu , nilipougua mkono
ulikuwa na stroko, lakini ilikuwa ni kama kitu cha ajabu kwasababu ilinijia
kwenye ndoto nikimuota mtu niliekuwa namjua, akitaka kunichanja chale kwenye
mkono wangu wa kulia, akidai kwamba yeye anatoa bahati, lakini nilijibizana nae
kwa muda nikikataa kunifanyia hivyo, gafla nilijikuta tayali ameshanichanja
chale nne kwenye mkono wangu wa kuume, lakini ilikuwa ndoto, niliipotezea
Ilipofika
asubuhi nikaanza kusikia mkono unauma sana, nikawa nakumbuka ndoto niloiota
lakini nikakumbuka kuuangalia mkono wangu nikakuta ni kweli kuwa chale zipo nne
kama nilivyoota. Kila dakika na kila saa iliyokuwa inapita mkono ulikuwa
unaendelea kuuma zaidi na kuzidi kuvimba, zilipita siku tatu hali ikiwa inazidi
kuwa mbaya. Kwa kipindi hicho, mama na baba walikuwa wameshaachana, na nilikuwa
kwa baba mama akiwa nyumban kwao, umbali wa km 8 kutoka nyumbani. Baba
alivyoona hali inazidi kuwa mbaya namshukur mungu kwa kuwa aliweka mbali
tofauti zake na mama ili niweze kupona kwanza. Kwa muda huo wote nilikuwa bado
sijamwambia baba mtu niliemuona kwenye ndoto.
Baba
aliniambia niende kwa mama bila kunipa nauli, nilitembea huku mkono ukiwa bado
unauma sana. Kitendo cha kuruhusiwa tu kwenda kwa mama niliamini kuwa nimepona.
Mama aliponiona aliumia na machozi yalimlenga machoni lakini alivumilia na hapo
mimi nilikuwa nalia tuu. Alinipa moyo kuwa nimepona. Sisi tumezaliwa na
kulelewa kweny maadili ya dini, tunamjua Mungu kuwa ni mtakatifu na
hachangamani na chochote lakin tulijalibu kutumia dawa nyingi sana za kienyeji
bila mafanikio yoyote na hapo ndipo mama aliposema sasa nimeshindwa.
Baada ya
siku zile tatu mkono uliacha kuuma na kuacha kuvimba, ukafa ganzi, hata mtu
angenifinya au kuukata nilikuwa sisikii chochote. Kweli tulimwamini Mungu
tukiomba saana, kwa imani ya Kikristo. Ilikuwa miezi mitatu mkono umepata
stroko, nikiwa najiona kuwa kilema hata nilipokuwa nikiomba nilikuwa sina imani
tena kama nitapona. Kulikuwa na sista mmoja katika shirika la mtakatifu
thelesia wa mtoto Yesu, alikuwa na mdogo wake aliekuwa na imani kubwa akimwamini
sana bikira maria aliemzaa Yesu, alikuwa mkoani dar es salaam, tulipewa namba
zake na kuwasiliana na kutuambia kuwa hana mpango wa kuja bukoba ila akatwambia
kuwa amepata dharula ya kwenda mkoani talime
Baada ya
hapo ikatubidi twende mwanza ili tukaonane naye , tulifikia kwa mjomba kesho
yake akarudi na kutupitia tulipokua, haombi sana wala hatumii njia yoyote
isiyoeleweka, ni sala tuu ila unazisali ndan ya siku tisa. Tangu nilippomuona
nilikuwa na imani kuwa nimepona na kweli siku ya nne tukiwa tunasali zile sala
mkono ulipona na nikaanza kuusikia na kuweza kukunja na kukunjua vidole, siku
ilofata niliamka nikaenda kanisan kumshukuru mungu, niliporudi nikajikuta
furaha yangu imerudi na nimepona kabisa, nikaendelea na masomo bahati mzur
tulikuwa bado hatujafanya mtihani wa moko, wiki mkono umepona iliangukia ijumaa
ikiwa j.tatu ni moko.
Nilifanya mtian
huo nikijua kuwa nitafeli, matokeo yalitoka mwezi wa kumi ikiwa imesalia wiki
moja tuanze mtiani wa taifa nikiwa na average 28, na average ilokuwa inatakiwa
ni 30, baada ya hapo sikuwa na muda wa kupumzika nikaanza kusoma kwa nguvu zote
yale walojifunza kipindi naugua, usiku na mchana badae tukafanya huo mtian
nikiwa na iman ya kufeli tuu na nyumban nishaambiwa nisipojitahidi uwezekano wa
kurudia hautakuwepo kulingana na kipato kilichokuwa kinapatikana kushindwa
kumudu mahitaji, tulifunga huo mwez wa kumi nikijalibu kufikilia ni kazi gan
nitafanya nikifeli. Nilijifunza kwanza kushona viatu badae nikaona haitatosha
kutimiza ndoto nilizokuwepo nazo, pili Nilijifunza kushona nguo maana nyumban
kulikuwa na chelehan akitumia mama japo ulikuwa kwa sili saana mama asijue,
badae nikaona nimejua ila ni vyema kuongeza fan maana nilikuw sijui ipi
itasaidia kutimiza ndoto zangu, niliendelea kushona huku nikijifunza kusuka
nywele, nikaona zinalipa saana na inaweza kuwa kazi yangu nikifeli.
Ilikuwa mwez
wa kwanza mwishon mwaka 2014, matokeo yakatoka huku nikijua kuwa sina shule
tena na kukutwa nimefauru japo sii vizur saana, nikiwa na average 33, nikapata
nafasi ya kuendelea na shule, huku nikisuka, nikishona viatu na nguo nilipopata
muda ikinisaidia kujilipia ela za tuition na madaftari, hadi nikamaliza form 4
nikiwa na malengo ya kuwa ness, matokeo yakatoka nikakutwa na ufauru wa
division 4 ya 29, huku hiyo likizo nikiendeleza fani ya kusuka, badae ndo
nikapata nafasi ya kujiunga na chuo cha utumishi wa umma tawi la tabora
nikichukua kozi ya utunzaji nyaraka na kumbukumbu, hapa ninapoandika ndo
nimemaliza ngazi ya cheti mwezi wa tisa mwenyez mungu atatenda nianze diploma.
Japo kwa
muda huo nikiwa chuo nilikuw nikisuka ili nimsaidie mama angarau ela ya
matumizi, hadi leo nasema hakuna mwanadam awezaye kuibadilisha kesho ya mwenzie.
Jina la bwana litukuzwe. Hadi hapo japo maisha yangu mimi ni ushuuda ila huo
ndo ulikuwa mzito saana jambo ambalo mwanadam aliona haliwezekan lakin mungu
akaamua kunitumia mimi kuidhihilisha nguvu yake, hata nilivyoenda chuo
nilijikuta hadi leo kila mtu ananiona mbalikiwa, maana ni wengi wanatafuta hata
kujua kimojawapo kiwasaidie kukidhi mahitaji ya kila iitwapo leo.
Ahsante mungu
maana unampango na mimi lazima utimie, bado ni kijana mdogo kama unavyoweza
kuniona kwenye picha, ninamiaka 19, nampenda Yesu, ahsante roho wa mungu kwa
kuniongezea hofu yako ndani ya moyo wangu, ahsante kwa hatua uliyonifikisha hii
leo, sikujua kama nitasoma nimalize secondary lakin nilimaliza kwa msaada wako,
sikujua kama nitapata chuo lakin wew ee mungu umetenda, baada ya kupata chuo
kama kawaida chuoni vishawishi ni vingi vinavyoweza kusababisha mtu kusahau
hali yake halisi ya nyumban alikotoka lakin huyu mungu anaendelea kupigana na
adui yetu shetan juu yangu ili nisipotee, japo naomba mwenyez mungu awasamehe
wale wote wanaotumiwa na shetan ili kuyakwamisha maisha yangu ,
Sasa hivi
niko likizo, naendelea kujitaftia hela ya matumizi, nauli na fungu la kumi,
nikisubilia mungu aendelee kujidhihilisha maana sikutarajia kama nitasoma
diploma maana hapakuwa na uwezekano lakin kila iitwapo leo anaendelea kufungua
njia kupitia kwa mama maana baba tangu mwaka 2014 alitutelekeza na kujikuta
anaishi peke yake na kumwachia mama mzigo mzito lakin mungu anasaidia kuna
mazingira yanayotengenezwa ili kuweze kupatikana ada ya kunisomesha, nikiungwa
mkono na ndugu zangu ambapo wamesema mama asihangaike kulipia hostel na chakula
wao watanisaidia huku na mimi nikijikwamua palipo na uwezekano, maombi yenu tuu
ndo yatakayofanya mimi nisonge mbele na hapo ndo mwisho wa ushuuda huu, bwana Yesu
apewe sifa.
AMEN!
Ndiyo, kama
nilivyoipokea ndivyo nilivyoiwasilisha, si et ee Mr.Meddy… ukweli ni kwamba
kuna wengi wana tatizo kama lako na leo hii wamepata kuiona njia uliyoitumia na
wao sasa wamepata uhakika wa kupona.
Najua hata
wewe unaesoma stori hii kuna mambo mengi makubwa umepitia au Mungu amekutendea basi ni wakati wako sasa wa kuwajenga wengine kupitia ukurasa huu, wasiliana nasi kwa
sim no. 0713 305 650
Nikushukuru
sana kwa kuwa pamoja name, hii ni tamati ya ushuhuda huu ila sio tamati ya
mambo ya muhimu kwako, hivyo kabla hujaondoka nakualika kutembelea vipengele
mbalimbali vya blog hii, na ufanye hivo kila siku.



4 Maoni
Enter your comment...nmependa sana ulivyoutumia mtandao Ubarikiwe sana;;; Tuko pa1 sana nakumbuka ishu hyo sana
JibuFutaUbalikiwe na wew kwa mchango wako basi share na wenhine wapwte kuiona njia
FutaUbalikiwe na wew kwa mchango wako basi share na wenhine wapwte kuiona njia
FutaMungu ni mkubwa
JibuFuta