Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

TRUE STORY | KUMBE MEDDY HAKUFA NA SASA NI MWANACHUO!

Habari Tanzania… Habari yako msaka hekima ndani ya Plan Media… Hapa ndipo nyumbani, nakukaribisha ndugu na jirani ili tushiriki nilichonacho kwa leo, na leo sasa nina Good News toka kwa Meddy Merchades.
Tuwekane wazi mpenzi msomaji, hivi unamjuaje huyu Yesu, unaamini nini kuhusu injili?, kabla hujanijibu nikukutanishe na shuhuda za matendo makuu ya Bwana aliyomtendea ndugu yetu, km nilivoipokea ndivo ninavoipost hapa chini>>>

USHUHUDA

Kwa jina naitwa meddy merchades, ni mwanachuo katika chuo cha utumishi wa umma, kwanza uzima wangu leo ni ushuuda tosha katika maisha langu, naomba nitakutumia ushuuda wangu. Ilikuwa mwaka 2013 nikiwa form two, mwezi wa tatu , nilipougua mkono ulikuwa na stroko, lakini ilikuwa ni kama kitu cha ajabu kwasababu ilinijia kwenye ndoto nikimuota mtu niliekuwa namjua, akitaka kunichanja chale kwenye mkono wangu wa kulia, akidai kwamba yeye anatoa bahati, lakini nilijibizana nae kwa muda nikikataa kunifanyia hivyo, gafla nilijikuta tayali ameshanichanja chale nne kwenye mkono wangu wa kuume, lakini ilikuwa ndoto, niliipotezea

Ilipofika asubuhi nikaanza kusikia mkono unauma sana, nikawa nakumbuka ndoto niloiota lakini nikakumbuka kuuangalia mkono wangu nikakuta ni kweli kuwa chale zipo nne kama nilivyoota. Kila dakika na kila saa iliyokuwa inapita mkono ulikuwa unaendelea kuuma zaidi na kuzidi kuvimba, zilipita siku tatu hali ikiwa inazidi kuwa mbaya. Kwa kipindi hicho, mama na baba walikuwa wameshaachana, na nilikuwa kwa baba mama akiwa nyumban kwao, umbali wa km 8 kutoka nyumbani. Baba alivyoona hali inazidi kuwa mbaya namshukur mungu kwa kuwa aliweka mbali tofauti zake na mama ili niweze kupona kwanza. Kwa muda huo wote nilikuwa bado sijamwambia baba mtu niliemuona kwenye ndoto.

Baba aliniambia niende kwa mama bila kunipa nauli, nilitembea huku mkono ukiwa bado unauma sana. Kitendo cha kuruhusiwa tu kwenda kwa mama niliamini kuwa nimepona. Mama aliponiona aliumia na machozi yalimlenga machoni lakini alivumilia na hapo mimi nilikuwa nalia tuu. Alinipa moyo kuwa nimepona. Sisi tumezaliwa na kulelewa kweny maadili ya dini, tunamjua Mungu kuwa ni mtakatifu na hachangamani na chochote lakin tulijalibu kutumia dawa nyingi sana za kienyeji bila mafanikio yoyote na hapo ndipo mama aliposema sasa nimeshindwa.

Baada ya siku zile tatu mkono uliacha kuuma na kuacha kuvimba, ukafa ganzi, hata mtu angenifinya au kuukata nilikuwa sisikii chochote. Kweli tulimwamini Mungu tukiomba saana, kwa imani ya Kikristo. Ilikuwa miezi mitatu mkono umepata stroko, nikiwa najiona kuwa kilema hata nilipokuwa nikiomba nilikuwa sina imani tena kama nitapona. Kulikuwa na sista mmoja katika shirika la mtakatifu thelesia wa mtoto Yesu, alikuwa na mdogo wake aliekuwa na imani kubwa akimwamini sana bikira maria aliemzaa Yesu, alikuwa mkoani dar es salaam, tulipewa namba zake na kuwasiliana na kutuambia kuwa hana mpango wa kuja bukoba ila akatwambia kuwa amepata dharula ya kwenda mkoani talime

Baada ya hapo ikatubidi twende mwanza ili tukaonane naye , tulifikia kwa mjomba kesho yake akarudi na kutupitia tulipokua, haombi sana wala hatumii njia yoyote isiyoeleweka, ni sala tuu ila unazisali ndan ya siku tisa. Tangu nilippomuona nilikuwa na imani kuwa nimepona na kweli siku ya nne tukiwa tunasali zile sala mkono ulipona na nikaanza kuusikia na kuweza kukunja na kukunjua vidole, siku ilofata niliamka nikaenda kanisan kumshukuru mungu, niliporudi nikajikuta furaha yangu imerudi na nimepona kabisa, nikaendelea na masomo bahati mzur tulikuwa bado hatujafanya mtihani wa moko, wiki mkono umepona iliangukia ijumaa ikiwa j.tatu ni moko.

Nilifanya mtian huo nikijua kuwa nitafeli, matokeo yalitoka mwezi wa kumi ikiwa imesalia wiki moja tuanze mtiani wa taifa nikiwa na average 28, na average ilokuwa inatakiwa ni 30, baada ya hapo sikuwa na muda wa kupumzika nikaanza kusoma kwa nguvu zote yale walojifunza kipindi naugua, usiku na mchana badae tukafanya huo mtian nikiwa na iman ya kufeli tuu na nyumban nishaambiwa nisipojitahidi uwezekano wa kurudia hautakuwepo kulingana na kipato kilichokuwa kinapatikana kushindwa kumudu mahitaji, tulifunga huo mwez wa kumi nikijalibu kufikilia ni kazi gan nitafanya nikifeli. Nilijifunza kwanza kushona viatu badae nikaona haitatosha kutimiza ndoto nilizokuwepo nazo, pili Nilijifunza kushona nguo maana nyumban kulikuwa na chelehan akitumia mama japo ulikuwa kwa sili saana mama asijue, badae nikaona nimejua ila ni vyema kuongeza fan maana nilikuw sijui ipi itasaidia kutimiza ndoto zangu, niliendelea kushona huku nikijifunza kusuka nywele, nikaona zinalipa saana na inaweza kuwa kazi yangu nikifeli.

Ilikuwa mwez wa kwanza mwishon mwaka 2014, matokeo yakatoka huku nikijua kuwa sina shule tena na kukutwa nimefauru japo sii vizur saana, nikiwa na average 33, nikapata nafasi ya kuendelea na shule, huku nikisuka, nikishona viatu na nguo nilipopata muda ikinisaidia kujilipia ela za tuition na madaftari, hadi nikamaliza form 4 nikiwa na malengo ya kuwa ness, matokeo yakatoka nikakutwa na ufauru wa division 4 ya 29, huku hiyo likizo nikiendeleza fani ya kusuka, badae ndo nikapata nafasi ya kujiunga na chuo cha utumishi wa umma tawi la tabora nikichukua kozi ya utunzaji nyaraka na kumbukumbu, hapa ninapoandika ndo nimemaliza ngazi ya cheti mwezi wa tisa mwenyez mungu atatenda nianze diploma.

Japo kwa muda huo nikiwa chuo nilikuw nikisuka ili nimsaidie mama angarau ela ya matumizi, hadi leo nasema hakuna mwanadam awezaye kuibadilisha kesho ya mwenzie. Jina la bwana litukuzwe. Hadi hapo japo maisha yangu mimi ni ushuuda ila huo ndo ulikuwa mzito saana jambo ambalo mwanadam aliona haliwezekan lakin mungu akaamua kunitumia mimi kuidhihilisha nguvu yake, hata nilivyoenda chuo nilijikuta hadi leo kila mtu ananiona mbalikiwa, maana ni wengi wanatafuta hata kujua kimojawapo kiwasaidie kukidhi mahitaji ya kila iitwapo leo.
 
Ahsante mungu maana unampango na mimi lazima utimie, bado ni kijana mdogo kama unavyoweza kuniona kwenye picha, ninamiaka 19, nampenda Yesu, ahsante roho wa mungu kwa kuniongezea hofu yako ndani ya moyo wangu, ahsante kwa hatua uliyonifikisha hii leo, sikujua kama nitasoma nimalize secondary lakin nilimaliza kwa msaada wako, sikujua kama nitapata chuo lakin wew ee mungu umetenda, baada ya kupata chuo kama kawaida chuoni vishawishi ni vingi vinavyoweza kusababisha mtu kusahau hali yake halisi ya nyumban alikotoka lakin huyu mungu anaendelea kupigana na adui yetu shetan juu yangu ili nisipotee, japo naomba mwenyez mungu awasamehe wale wote wanaotumiwa na shetan ili kuyakwamisha maisha yangu ,

Sasa hivi niko likizo, naendelea kujitaftia hela ya matumizi, nauli na fungu la kumi, nikisubilia mungu aendelee kujidhihilisha maana sikutarajia kama nitasoma diploma maana hapakuwa na uwezekano lakin kila iitwapo leo anaendelea kufungua njia kupitia kwa mama maana baba tangu mwaka 2014 alitutelekeza na kujikuta anaishi peke yake na kumwachia mama mzigo mzito lakin mungu anasaidia kuna mazingira yanayotengenezwa ili kuweze kupatikana ada ya kunisomesha, nikiungwa mkono na ndugu zangu ambapo wamesema mama asihangaike kulipia hostel na chakula wao watanisaidia huku na mimi nikijikwamua palipo na uwezekano, maombi yenu tuu ndo yatakayofanya mimi nisonge mbele na hapo ndo mwisho wa ushuuda huu, bwana Yesu apewe sifa.

AMEN!

Ndiyo, kama nilivyoipokea ndivyo nilivyoiwasilisha, si et ee Mr.Meddy… ukweli ni kwamba kuna wengi wana tatizo kama lako na leo hii wamepata kuiona njia uliyoitumia na wao sasa wamepata uhakika wa kupona.

Najua hata wewe unaesoma stori hii kuna mambo mengi makubwa umepitia au Mungu amekutendea basi ni wakati wako sasa wa kuwajenga wengine kupitia ukurasa huu, wasiliana nasi kwa sim no. 0713 305 650


Nikushukuru sana kwa kuwa pamoja name, hii ni tamati ya ushuhuda huu ila sio tamati ya mambo ya muhimu kwako, hivyo kabla hujaondoka nakualika kutembelea vipengele mbalimbali vya blog hii, na ufanye hivo kila siku.

Chapisha Maoni

4 Maoni

  1. Enter your comment...nmependa sana ulivyoutumia mtandao Ubarikiwe sana;;; Tuko pa1 sana nakumbuka ishu hyo sana

    JibuFuta
    Majibu
    1. Ubalikiwe na wew kwa mchango wako basi share na wenhine wapwte kuiona njia

      Futa
    2. Ubalikiwe na wew kwa mchango wako basi share na wenhine wapwte kuiona njia

      Futa