Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

BAISA AWAONYA WAIMBAJI WANAO KATA TAMAA

Baisa Mhela ambae ni muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania anaekuja kwa kasi awaonya waimbaji wanaokata tamaa, amesema waimbaji wengi wanaochipukia wanakosa nguvu ya kufanya huduma hiyo kutokana na sababu mbalimbali lakini ukizitazama sababu zote hizo ni sababisho la shetani ili kuzuia huduma ya Mungu.
Aidha ameendelea kusema ukitazama sababu kubwa zinazowafanya waimbaji kukata tamaa ni gharama za kulipia studio,Nauli,Mavazi na hata kukatishwa tamaa na wanaomzunguka, akaonya kwa kusema kuwa waimbaji wanapaswa kujitambua na kuelewa kuwa wanafanya kazi ya Mungu na kikubwa Mungu wetu ni tajiri hakosi kitu na wala hashindwi kitu hivyo wakiomba kwa mwenye kazi yake hatowanyima kamwe.
Ameongeza kwa kusema kuwa hata biblia inaeleza wazi jinsi Yesu alivyowauliza wanafunzi wake kwamba "Je,mlipungukiwa na kitu nilipowatuma bila kitu, bila mkate,bila mavazi na wanafunzi wakamjibu hapana" maana yake Mungu anapokutumia kutangaza neno lake kama ulivyo na hatokuacha atakulisha, atakuvisha na atakujaza vyote baada ya kuona hekima yako na utayari wa kuyapokea.
Amemalizia kwa kuwaonya waimbaji wote, Wachungaji,Wainjilist, Maasikofu, Mitume na Manabii ama watumishi wa Mungu kwa ujumla kuto vaa sana ubinadamu bali wayapokee yote kama razalo mtumishi wa Mungu katika biblia takatifu.

Chapisha Maoni

0 Maoni