Hatima ya mchezaji wa kiungo wa Singida United Deus Kaseke na mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa kujulikana alihamisi ya wiki ijayo baada ya kikao cha kamati ya saa 72 kukutana. Wachezaji hao walisimamishwa kutokana na tuhuma za kuleta fujo katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu msimu uliopit kati ya Yanga na Mbao Fc.Hata hivyo afisa habari wa TFF Alfred Lucas alisema kikao hicho kitatoa maamzi juu ya suala hilo "Kikao kimdchelewa kwasababu ya uchaguzi na kubadiliswa kwa kamati za TFF, lakini mtakumbuka wachezaji hao walisimamishwa kwenye mechi ya mwisho msimu uliopita"
Kutokana na adhabu hiyo Kaseke alikaa jukwaani wakati Singida United ikipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mwadui, Vivyo hivyo kwa Mzambia Obrey Chirwa aliyeshindwa kuichezea Yanga katika mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya mahasimu wao Simba Sports Clab ambao ulimalizika kwa sare ya kutokufungana na ule mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Lipuli kutoka Iringa ambao ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 katika uwanja wa uhuru jijini Dar Es Salaam.

0 Maoni