Hii ni historia fupi ya muimbaji wa nyimbo za injili
Tanzania anakuja kwa kasi ndugu Yoshua Mbonabucha maalufu kama Bishop Joshua ni
muimbaji ambae amejaaliwa kipaji na sauti yenye mvuto na uwezo wa kutunga
nyimbo zenye ujumbe mzuri na uoako katika kuihubili injili kamili ya Mungu.
Muimbaji huyu alianza rasimi uimbaji wake mnamo mwaka 2014
ambapo alikua akiimba muziki wa kidunia au mziki wa starehe za dunia yaani
muziki wa kizazi kipya [Bongo fravour] alifanya muziki huo kwa muda wa mwaka
mmoja na kujizolea umaalufu katika muziki huo japo lilikua siyo kusudio la
Mungu kuimba muziki huo.
Mnamo mwaka 2015 aliamua kuacha muziki wa kidunia ndipo
aliokoka na kujiunga kwenye kwaya ya kanisa la E.A.G.T MPIJI MAGOHE mkoani Dar
es salaam akaendelea kumtumikia Mungu kwa njia ya umbaji alipokelewa vizuri na
uongozi wa kanisa wakamlea kiroho ndipo alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwaya
katika kanisa hilo.
Mnamo mwaka 2016 aliamua kuimba kama muimbaji binafisi ndipo
aliamua kuanza kurekodi nyimbo tano ambazo kiukweli ni nyimbo ambazo
ukizisikiliza zina ujumbe kamili kuanzia majina ya nyimbo hizo ujumbe na hata
sauti yake ya uimbaji wake miongoni mwa nyimbo hizi ni hizi zifuatazo hapa
chini;
1:MKONO WA BWANA
2:IMANI
3:AMINI
4:DAKIKA 90 na
5:KWA NEEMA
Mwaka huu amebahatika kukamilisha albam kwa kurekodi wimbo
mmoja ambao unafanya vizuri katika ulimwengu wa injili kwa hivi sasa
unaofahamika kwa jina la MWAGA BARAKA na wimbo huu ndio umebeba jina la albam
na albam hii ipo katika mfumo wa audio.
Ukizihitaji nyimbo hizi znaatikana katika mfumo wa Adio CD
na mitandao ya kijamii kama google account yake ya mbonabuchajoshua@gmail.com au
WhatsApp namba yake ya 0714598392 ukifanya mawasilianohayo unajipatia nyimbo
zote hizo naamili utabarikiwa nazo.
Muimbaji huyu yuko tayari kwa miaaliko mbalili mbali ya
kanisani matamasha n.k hivyo kama unahitaji aje kuhudumu mahali ulipo yupo
tayari kufika ili kuihubiri injili kamili ya Mungu chakufanya ni kuwasiliana
nae kwa namba 0714598392.
Bishop Joshua ameshawahi kuhudumu katika matamasha tisa na
mikutano ishirini na moja badhi ya
matamasha aliyo hudumu ni uzinduzi wa Maria Matha Charles albamu ya Kwaanini
Mimi,Uzinduzi wa albamu ya Deborah Kihanga ya Nimemuona Bwana n.k
Bishop Joshua anamshukuru Mungu ndugu jamaa na marafiki kwa
kumwezesha kufika katika hatua aliyoifikia vilele anaomba kwa taasi,kampuni au
mtu mwenye uwezo wa kumsaidia kufanya video ya albam hii kwakua yeye hanauwezo
wa kulipa gharama hiyo kwa sasa ukilinganisha yeye bado ni mwanafunzi wa kidato
cha sita hivyo ukiguswa na huduma hii mtafute ili kuifikisha injili mahali
inapotakiwa kufika kupitia huduma aliyonayo kijana huyu.

0 Maoni