Wakazi wa Buguruni Mkoani Dar es salaam walalamikia ulinzi na usalama ambapo hukabwa na kuporwa mali zao nyakati za usiku na alufajiri.
Wakati wa mahojiano na mwandishi wetu Bw.Adam Nyota Adam ameiambia plan media kuwa tatizo la vibaka katika mtaa wao ni tatizo sugu linalo wasumbua wakazi hao hasa waendapo kazini nyakati za alfajiri na hata warudipo majumbani nyakati za usiku ambapo hupigwa mpaka kujeruhiwa na kuporwa mali zao.
Pia Bw.Haruna Selemani ameiambia plan media kuwa vibaka hao wamebuni mbinu mpya ambapo huvalia mavazi ya kike ili kutokufahamika akaongeza kwa kusema kuwa vibaka hao si wa mtaa huo bali hutoka maeneo ya Kigogo,Tabatata,Bizuu,Ngongolamboto n.k.
Mwandishi wetu amemtafuta mwenyekiti wa mtaa Bw. Karim Malapa amekiri kuwepo kwa tarizo hilo na kukanusha kwamba wezi ni wakazi wa mtaa huo na kama wanatoka njee ya mtaa basi wanawafata wenyeji wa mtaa hivyo wanapata tabu kuwakamata mchana kwa kukosa ushahidi wa kutosha.
Aidha Bw. Malapa amesisitiza kuwepo na ulinzi shirikishi kwani polisi kata wapo wachache hivyo hupata shida kufanya doria katika mitaa yote nakuongeza kusema kuwa ulinzi shirikishi uliopo ni watu wanaojitolea.
Pia Bw. Malapa ameomba wananchi na serikali ya mtaa kuweka vikao kwa ajili ya kujadili kuwepo na malipo kwaajili ya ulinzi shilikishi katika mitaa yote.
Bw.Malapa amemaliza kwa kuiomba serikali kuu kwa kutenga mishahara ya kuwalipa walinzi wadoria za usiku kutokana na polisi kata kuwa wachache na kushauri kuwa wanachi wawe watulivu serikali yao inafanyia kazi kero hiyo ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani nyakati zote.

0 Maoni