KIMBUNGA CHAUA
WATU SABA
Kimbunga
chasababisha uharibufu mkubwa katika eneo la Caribbean ambapo mali nyingi zimeharibiwa na kimbunga
hicho ikiwemo kupelekea watu saba kupoteza maisha , kimbunga hicho kinacho
fahamika kwa jina la Irma kilikumba kisiwa hicho na kusababisha watu washindwe
kuishi huku maafisa wakionya kuwa maeneo ya kisiwa cha ST.Martin kinacho
milikiwa na uingereza kimeharibiwa kabisa.
Jitihada za uokoaji zinagonga mwamba kutokana na ugumu wa kupata maeneo mengine, wakati huo huo upepo umekua na nguvu na kuzalisha vimbunga viwili, kimbunga hicho cha kiwango cha tano kinatajwa kuwa ni kiwango cha juu na sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico.
Nusu ya
wakazi wa Puerto Rico hawana umeme baada ya kimbunga hicho kusababisha mvua
kubwa inayo ambatana na upepo mkali huku
maafisa wakisema huenda umeme ukawa tatizo kwa siku kadhaa, Kimbunga hicho
kilikua na kasi ya kilomita 295 kwa saa ambapo kilikadiliwa kupita katika pwani
ya Dominica .



0 Maoni