WATU
WANNE WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUJIUNGA NA AL-SHABAB
Jeshi la
polisi nchini Kenya linawashikilia raia wanne kutoka nchini Burundi
wanaodhaniwa kuwa walikua wanaelekea nchini Somalia kujiunga na kundi la
kigaidi la Al-Shabab, Maafisa wa ujasusi walikuwa wakiwafuatilia raia hao baada
ya kupata taarifa kuhusu mipango yao, kwa mjibu wa msemaji wa polisi George
Kinoti.
Ameongeza
kwa kusema washukiwa hao wanne walikamatwa katika kizuizi cha polisi mjini
Isiolo kilometa 350 kasikazini mwa mji wa Nairobi wakielekea mpakani mwa mji wa
Mandera.
Pia maafisa
wa ubarozi wa Burundi mjini Nairobi wanasema watatoa taarifa kamili kuhusu
kukamatwa kwa raia hao wanne baada ya kushauriana na mamlaka husika katika nchi
ya Kenya
Tukio kama
hili si lakwanza kutokea nchini Kenya, mnamo mwezi
Janury mwaka 2017 raia wa kigeni kutoka nchi ya Tanzania alikamatwa katika
mji wa Mandera alipokua akijaribu kuvuka mpaka kuelekea Somalia kwa lengo la
kujiunga na kundi lakigaidi la Al-Shabab.


0 Maoni