SURUHISHO LA AJIRA KWA VIJANA TANZANIA
Karibu
katika makala fupi ya leo ambayo nimekuandalia naamini unaenda kujifunza kitu
kipya kupitia makala hii na kama unajua basi nakuongezea maarifa zaidi, mada ambayo tunayo izungumza katika siku ya
leo ni ajira kwa vijana wa kitanzania na hata wasio watanzania pia inawahusu
kwasababu suala la ajira halitofautiani sana katika nchi zetu hususa ni za ki
afrika. Karibu katika somo la leo na kama utakua na maoni au ushauri
utatuandikia hapo chini mwishoni mwa makala hii.
Ajira nini?
Ajira
ni shughuli harari anayo ifanya binadamu kwa ajili ya kumuingizia kipato au
malipo yanayo lingana na shughuli husika anayoifanya binadamu huyo, hii ni
maana moja ya neon ajira japo kuna maana nyingi za neon hilo ila kulingana na
muda naomba tutumie maana hii na kama una maana nyingine ya neon hilo siyo
dhambi ukiitumia ilimladi tusipoteze maana.
Kuna
aina mbili za ajira ambazo ni kujiajiri na kuajiriwa nisikupotezee muda kwa
kuelezea kiundani maana ya hizi aina za ajira huu ulikua ni utangulizi wa
kukuweka karibu ili kukuweka karibu kwa kile ambacho naenda kukizungumza siku
hii yaleo.
Niombe
radhi kwa waajiri wote popote mlipo
kwakua leo nataka nitete na vijana wenzangu kuwa na mawazo ama kujikita zaidi
katika suala la kujiajiri kuliko kutegemea saana kuajiriwa naamini vijana mko
na mimi katika hili lakini simanishi ndo muache kuajiriwa hapana soma kwa
makini na taratibu utanielewa nini namaanisha.
Tatizo
la ajira limekua tatizo kwa sisi vijana hasa vijana wakitanzania na hiki ndicho
kimenipelekea kuandaa makala hii ili vijana wenzangu muweze kuamka na kutambua
ni jinsi gani ya kupambana na hali hii ya tatizo la ajira kwetu sisi vijana.
Tatizo
la ajira halipo Tanzania tu bali lipo mataifa mengi tu na hata mataifa yale
mnayo yasifu kuwa yameendelea sitaki nielezee sana kati mataifa mengine kwakua
leo tunazungumzia taifa letu hivyo kama ulikua hujiui chanzo kikubwa cha tatizo la ajira Tanzania
basi jua kuwa ni mfumo wa elimu tuliokuwa nao.
Niombe
radhi kwa Mh. Ndalichako maana hii ni wizara
nyeti ila naomba tu kwa leo nijaribu kuwaelewesha watanzania, ni ukweli
usiopingika kuwa mfumo waelimu tulionao ni chanzo kikubwa cha tatizo la ajira
Tanzania najua kuna wasomi wakubwa sana mna PHD mnaanza
kubisha kwa ninachokiongea leo maana mwenzenu sikupata nafasi ya kusoma saana
japo nina elimu ya asili .
Nikushukuru baba mwenye nyumba kwa kutuletea elimu bure
bila kusahau kauri mbiu yako nzuri unayoitumia ya hapa kazi tu! Naile ya “serikali ya viwanda” Kwa mjibu wa kitabu cha Mungu
niinachokitumia kinasema “asiefanya kazi na asile”
kwa maana hiyo asie fanya kazi akila anakua ametenda dhambi.
Elimu
bure wazazi mmejitahidi kupeleka watoto shule nikijaribu kutembelea shule
kadhaa nakuta shule zimejaa wanafunzi kuanzia darasa lakwanza mpaka kidato cha
nne ila naasikia wasome wakijua serikalini hakuna ajira siwatishi wazazi ambao
mna watoto wanao soma leo nimeamua niwaletee dawa ya tatizo la ajira kwa vijana
wa kitanzania basi usichoke soma mpaka mwisho upate dozi kamili.
Katika
mfumo wa elimu tunao utumia kwa sasa ni kuanzia Chekechea[Nursary],msingi[Primary],Sekondari[Secondari]
pamoja na Vyuo[Coledge & Univercity] huu ndio mfumo ambao huwa
unatumika katika kuwatengeneza vijana kuwa wasomi ikizingatiwa kwa sasa elimu
ya msingi na sekondari ni bure hivyo tunapata vijana wengi wasomi wasio na
ajira hapo baadae kama hatutofunguka macho mapema.
Katika
mfumo huu wa elimu haumjengi kijana katika kujiajiri bali mfumo huu unamjenga
kijana katika mazingira ya kuajiriwa walimu wenzangu mtakua mashahidi wa
hilli maana sisi ndio hushinda na vijana
hawa na hatimae tunakua tunazalisha vijana ambao hawna mawazo ya kujiajiri
kulingana na mitaala na mfumo huu unao tuimika kwasasa.
Lazima
tutambue kuwa zama zinabadilika miaka ya nyumba sana kulikua na mazoea kwamba
mtu anapokua amesoma basi ajira zinakua njenje kwakua kulikua na uhitaji mkubwa
wa wafanya kazi, katika zama hizi nikwamba idadi ya wasomi imeongezeka ofisi ni
zilezile hivyo inakua ngumu kila mtu kupata nafasi ya kazi kama iliovyokuwa
zamani vilevile idadikubwa ya wasomi inapelekea wasomi wengi kukosa nafasi za
kazi na kubakia mtaani.
Lazima
tukubari kuwa tunaudhaifu wa sekta husika ikiwemo na sisi raia wenyewe bila
kusahau wazazi mnao wasomesha watoto wenu kuwa hakuna mfumo elekezi wa
kuwajenga watoto ama wanafunzi katika kuwajengea mawazo na ujuzi wa kuweza
kujiajiri mala baada ya kuhitimu elimu yao hivyo ni muda sasa wa kubadilika na
kutambua udhaifu huo.
Juzi
wakati nikiwa kwenye daladala nilikutana na kijana mmoja mwenye umri wa miaka
25 akiwa ameshikiria bahasha ya kaki alikua amevaa nguo safi na kiatu kizuri
sana lakini kwa mbaali alionekana kama
amechoka hivi kwa bahati nzuri nilikaa
siti ya karibu yake nilimsalimia akaniitikiasalammu yangu ndipo nikapata nafsi
ya kuzungumza nae nikamuuliza kaka unafanya kazi ofisi gani? Akajibu”sina kazi” nikamuuliza umetoka wapi? Akajibu “nimetoka ofisi Fulani (sipendi niitaje kwasababu
za kiusalama) akaendelea kusema nilikua nimepeleka
barua ya kuomba kazi lakini imeshindikana na ni mwaka watatu natafuta kazi
chaajabu sijapata, nimemaliza chuo mwaka juzi na haya mavazi unayoona nimevaa
nimeazima kwa rafiki yangu yani hii nchi we acha tu” tuliendelea kuongea
nae mambo mengi kaka yangu yule hatimae nikafika kituo kilichofatia nikashuka
yeye akaendelea na safari yake huu ni mfano tu ila naamini tuna vijana wengi
sana wa aina hii naamini mmeanza kunielewa sasa.
Naongeqa
na wewe kijana mwenzangu, kaka yangu, mdogo wangu na hata nyie wazazi wetu mnao
tusomesha juu ya tatizo la ajira kwa vijana, hebu tujifunze kwa mataifa mengine
yaliyo endelea kwamba wao walifanikiwa vipi katika hili utakuta kwamba wao
wametengeneza mifumo mizuri ya kuwajenga vijana wao katika mazingira ya
kujiajiri kuanzia ngazi ya familia na hasa kati umri mdogo.
Nikisema
kuwajenga vijana katika mazingira ya kujiajiri wengine hawanielewi na wengine
wateleta sababu kwamba wazazi wenyewe wana miaka kedekede wakiwa katika kazi za
kuajiriwa na watawezaje kuwajengea mazingira ya kujiajiri watoto wao na hali
kuwa kipato chao ni duni? Hili ni swali ama hoja ambayo haina msingi wowote,
kwa imani yangu ni kwamba inawezekana kama unafatilia makala hii kwa makini.
Lakini
pia mfumo wa elimu katika nchi yetu unaangalia mtu amefauru nini? na siyo mtu
anajua nini? hivyo mtu anapo fauru mtihani haijalishi amekariri huhesabiwa
mojakwamoja anafaa hivyo mtu anapo fanya vibaya katika mtihani haijalishi
anaweza na anajua nini? mojakwa moja huonekana hana kitu kichwani jambo ambalo
siliamini sana na ndo chanzo kikibwa cha watu kukosa ujuzi wakufanya mambo
mengine hasa kujiajiri jambo ambalo ni tofauti na mataifa yaliyo endelea.
Katika
uumbaji Mungu alimuumba kila mwanadamu kwa jinsi ya pekee na kipaji ama uwezo
wapekee wakufanya jambo fulana na kwa bahati mbaya hatuna utamaduni wa
kuthamini vipaji vya watoto wetu wakati hivi ndivyo vingeongeza uwezo wa vijana
wetu kujiajiri kwakua mtu anakua anafanya kitu ambacho anakiweza na anakipenda
yani kwa uwezo aliojaliwa na mwenyezi Mungu.
Nisielezee
sana suala vipaji maana siyo somo la leo ila nilikua nataka nikuvute karibu
uweze kunielewa kwa undani kipi nazungumza japo kipaji ni sehemu ya mtu
kujiajiri, kuna furusa nyingi sana ambazo zinatuzuynguka vijana katika nchi
yetu ya Tanzania kwamfano kilimo na ujasilia mali kwa ujumla lakini pia kuna
furusa nyingi tu hapo ulipo sema hujadhamilia kuzifanyia kazi.
Kilimo
ni sekta pana sana ambayo inaweza kubeba ajira maelufu kwa vijana tatizo kubwa
nikwamba vijana wengi na hasa wasomi hawana mawazo ya kugundua kama kilimo
kinalipa sana, enzi za mwalimu J.K. Nyerere
alianzisha kauli mbiu ya kilimo ni uti wa mgongo ambayo kwasasa imebaki kuwa ni
hadithi, nahii sababu kubwa ni mchango wa serikali katika hili kwasababu wakati
mkulima analima serikali haipo akivuna
tu serikali inaanza kuonekana hivyo hupelekea vijana kuona kilimo hakina
manufaa kwao hatimae siku hizi wazee na kina mama ndio utawakuta kwenye masuala
ya kilimo.
Vilevile
vifaa vinavyo tumika ni duni ambavyo sanasana ni majembe ya mkono na kupelekea
vijana wengi kuchukizwa na kufanya kazi za kutumia nguvu sana lakini pia vifaa
na pembejeo bado ni tatizo kubwa, nisielezee sana kuhusu kilimo maana lengo
letu ni kupata suruhu ya tatizo la ajira kwetu vijana.
Ifike
muda tuzione changamoto tulizo nazo na kuweza kupambabna nazo na siraha peke ya
kupanda na hali hii ni mawazo chanya kwetu sisi vijana na hasa ikizingatiwa
walio wengi mnajiita wasomi kutokana na vyeti mlivyo vipata vyuoni , nijambo la
kushukuru kwakua tumeishia darasa lasaba, basi tumalizie kwa kuangalia vitu
gani tufanye ili tujiajiri.
MAMBO YA KUFANYA ILI KIJANA KUJIAJIRI
Haya
ni baadhi ya mambo ambayo kijana akiyafanya anaweza kujiajiri kwa kutumia mtaji
aliokuwa nao maana mtaji wakwanza ni afya njema na akili au mawazo ulivyo
jaliwa na Mungu tangia pale ulipo zaliwa na asmini kuwa mtaji ulio nao hakuna
tajiri mwingine duniani mwenye nao karibu sana soma kwea makini uelewe usipo
elewa unaruhusiwa kuuliza name nitakujibu haraka iwezekanavyo.
1:Weka cheti pembeni
Simaanishi
ukitupe cheti chako lahasha maana kitahitajika mala baada ya kukamilisha
malengo yako ya kujiajiri, maana yangu kubwa nikwamba ukitaka kujiajiri usiangale
thamani ya cheti ulichonacho kwasababu utashindwa kuchukua uamzi huo wa
kujiajiri maana cheti chako kitakutaka upate kazi kwenye kiti cha kuzunguka
kuingia kazini saa 2 asubuhi na kutoka saa 9 mchana.
2:Angalia furusa ama kile unacho kipenda
Inabidi
uangalie furusa iliyopo katika mazingira uliyonayo kuzunguka au lazima uangalie
kilichopo ndeni yako au kipaji ama kile unacho kipenda, kwani kile
alichokuwekea Mungu ndani yako alikua na kusudi la wewe kufanikwa hivyo
ukifanya kinyume utajishangaa unazeeka ukiwa hujafanikiwa hata kidogo na hiki
ndicho wengi hawakifahamu na wengi wao wanakaa na kupiga kelele kwamba maisha
magumu na hali kuwa utajiri undani yao.
3:Chagua furusa
Lazima
uchague furusa moja wapo amayo unaona kwamba itakufaa katika kuzishi ndoto zako
maana utakapo kosea kuchagua itakusababishia kutozifikia ndoto zako maana
utakua unafanya kitu ambacho unajilazimisha na hueendani nacho hivyo ni vizuri
ukawa makini katika kuchagua hiyo furusa ili uweze kuziishi ndoto zako.
4:Fanya uchunguzi
Baada
ya kuchagua hiyo furusa inabidi uifanyie uchunguzi kwa wengine ambao wanaifanya
na kama karibu yako haipo kubali kuingia gharama za kwenda waliko kufanya
uchunguzi huo na ikishindikana kabisa jaribu kutumia mitandao maana siku hizi
tumerahisishiwa mambo itakusaidia kupata jawabu kwa haraka na vyepesi kusonga mbele katika kuifanyia kazi furusa
yako.
5:Fanya tathimini
Baada
yakuona kuwa furusa hiyo inakufaa fanya tathimini kwamba je,furusa hiyo
itakulipa au utaonekana tu kuwa umejiajiri pasipo kufaidika na furusa yako?
hili ni jambo la msingi maana tunajiajiri ili tufaidike na tunacho kifanya na
ndo maana kubwa ya kujiajiri, hivyo inakupasa kuwa makini katika hili kwa
manufaa yako.
6:Chukua maamzi
Baada
ya kugundua kama furusa inakulipa unapaswa kuchukua maamzi magumu ya kufanya
kazi kwa kuthamiria maana kwa kila jambo ni lazima kuchuka maamzi ili
kulifanikisha maana hakuna kazi inayo fanyika pasipo kuiamru akili yako kufanya
maamzi.
7:Tenga muda maalumu
Baada
ya kuamua unapaswa kutenga muda wa kufanya kazi zako usikubali kupoteza muda
wako bure na kama ukishindwa kuzingatia muda utashangaa mambo hayaendi kwakua
utakua umeshindwa kuzingatia na kuheshimu muda wako, wahenga walisema muda ni mali
hivyo muda nao ni sehemu ya kukufanya ufanikiwe katika kazi zako.
8:Thubutu
Baada
ya kuheshimu muda sasa ni kazi inaanza maana mpaka hapo umesha elewa kwamba
unafanya kazi ambayo unaamini itakufikisha pale unapohitaji kufika na
ikizingatiwa kwamba unafanya kitu ambacho unakipenda kwa moyo wako wote na
Mungu atili baraka zake katika kazi yako.
9:Bidii
Baada
ya kuifanya hiyo kazi usiishie kuifanya tu bali lazima ujibidishe maana bidii huleta uvumilivu na mafanikio maana
vijana wengi wanapenda kazi za kulalka masikini na kuamka tajiri ila
nakuhakikishia kwamba hakuna kazi harari ya hivyo isipokua kazi haramu ambazo
zinamchukiza Mungu na watu ambazo huwapeekea wengi kupotezamaisha mapema mno.
10:Kuwa na kisi
Hii
ni sehemu yenye utata kidogo maana vijana wengi hatuna kiasi cha kufanya mambo
yetu kwamfano watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwasababu ya anasa na ninapo
zungumzia anasa hili ni suala pana ambalo nisinge penda kulizungumza kiundani
kwa leo, ninapo zungumza uwe na kiasi namaanisha matumizi yako ya Chakula,Malazi
na Mavazi visizidi uwezo wa kipato chako maana utashindwa kuiendeleza kazi yako,
hivyo unapaswa uwe na kiasi katika hayo.
Na
huu ndio mwisho wa makala yetu kwa leo naamini kuna mambo umejifunza na
kuongeza maarifa ila usikose katika somo litakalo fuatia chakufanya ni
kuendelea kutembelea mitandao yetu ili usipitwe na somo lijalo vilevile kama
unahitaji nakala ya somo hili inapatikana chamsingi ni kuwasiliana nasisi tuone
jinsi gani ikufikie namba ya kuwasilana nasisi ni 0713305650.
Kwa
maoni au ushauri tuandikie hapo chini au tuandikie kupitia email yetu planmediatz@gmail.com ama namba yetu ya simu
0713305650 itakua vizuri sana hii ni Plan Media way to success.
TANGAZA NA PLAN MEDIA KWA BEI NAFUU SANA
TEL: +255 713 305 650
EMAIL: planmediatz@gmail.com
WOTE MNAKARIBISWA








0 Maoni