WAKIMBIZI
WAISHIO TANZANIA WAANZA KUREJEA NCHINI BURUNDI
Wakimbizi kutoka nchini Burundi
waishio Tanzania mkoani Kigoma katika kambi ya Nduta Wilayani Kibondo waanza kurejea nchini kwao leo hii ikiwa ni
makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Burundi.
Wakimbizi 302 ndio walio rejea siku
ya leo ikiwa ni awamu yakwanza ya kampeni ya kuwarejesha wakimbizi takribani
elfu12 kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2017.
Wakimbizi hao wamesafirishwa kwa
kutumia usafiri wa mabasi mpaka nchini Burundi, Tanzania imekua ni nchi
inayohifadhi wakimbizi wengi kutoka Burundi na Kongo kuliko nchi nyingine
katika ukanda wa Afrika mashariki.
Kwa mjiu wa taarifa ya shirika la wakimbizi
duniani UNHCR iliyotolewa mwezi juni, kufikia wakati huo kulikua na wakimbizi
241,000 kutoka nchini Burundi huku
asilimia 60% ya idadi hiyo ikiwa ni watoto


0 Maoni