NA .GOOGLUCK
CHRISTOPHER
Rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania Dk. Joseph Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya
shirika la kuzalisha umeme Tanzania [TANESCO] lililopo jijini ni Dar es salaam
kuwekewa alama ya ‘X’ kuashiria jingo hilo kubomolewa, Rais ameyasema hayo
katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara katika eneo la Ubungo.
Aidha Rais ameongeza kwa kusema
kuwa Jengo jingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji
ambalo lipo jirani na jingo hilo la shirika la kuzalisha umeme Tanzania TANESCO
katika ineo hilo la Ubungo..
Vilevile Raisi ametoa
agizo hilo kutokana na majengo hayo kujengwa
ndani ya hifadhi ya barabara, Zoezi la bomoa boma limekuwa likiendelea,
ambapo majengo pembezoni ya barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na
maeneo mengine ya nchi yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika
maeneo yanayodaiwa kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.


0 Maoni