NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Mratibu
wa kwaya ya vijana kanisa la [KKT] ushirika wa Hananasifu jijini Dar es salaam
Bw. Hemeid Msairi Gembe ameeleza sababubu zinazo wafanya baadhi ya waimbaji wa
nyimbo za injili Tanzania kukimbia
vikundi vya uimbaji makanisani maalufu kama Kwaya kuwa ni masirahi binafisi.
Aidha
Bw. Gembe ameieleza Plan Media kuwa ubinafsi
umewatawala baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili na kujali masirahi
binafsi kwasababu ukifuatalia waimbaji wa nyimbo za injili wanao fanya vizuri
chimbuko lake walianza kwenye kwaya lakini baada ya kufanikiwa wanasahau waliko
anzia.
Vilevile
Gembe amesema waimbaji wengi wanapo zindua albam fedha yote inaingia mfukoni
mwao huku kwaya ikizindua albamu fedha inaingia katika mfuko wa kwaya ili
kuendeleza huduma katika sehemu mbalimbali hii huwafanya waimbaji kuona kuwa
hawafanikiwi na huduma hiyo.
Gembe ameongeza kwa kusema kuwa muimbaji
akishaweza kuimba na kuandika mashairi ya nyimbo hizo za injili anaenda
kurekodi wimbo wake binafisi na kusema hili ni jambo jema lakini wimbo huo
ukifanya vizuri ndo haonekani tena kwenye kwaya na ukimuuliza atakwambia huduma
imembana.
Pia
Gembe amesema unakuta waimbaji wa kwaya wanapo hitajika wanatumia gharama zao
wenyewe mpaka kumaliza huduma lakini waimbaji baadhi yao huwa wana gharamiwa
hivyo huona kwamba hii ni njema kwake hivyo wanasahau kuwa wanapoteza maana ya
kumtumikia Mungu wanapo fanya hivyo.
Hata
hivyo Gembe amesema kuwa hii inasababishwa na waimbaji wenyewe kutokuwa na
misingi mizuri ya neono la Mungu ndani yao hivyo wanakosa kuwa waaminifu kwa Mungu kwasaba neono
la Mungu linasema “Fedha na Dhahabu vyote ni mali ya Bwana” na kama
wakimtumikia kwa uaminifu basi hivyo
vitakua vyao.
Vilevile
Gembe ametoa ushauri kwa waimbaji wa nyimbo za injili kusoma neon la Mungu kwa
wingi waache kusoma mstari mmojammoja na badala yake neono kwasababu Biblia
kitabu kinacho jieleza vyakutosha sana
na wasiwe watu wenye tamaa ya pesa na wakumbuke kuwa tamaa ni dhambi.
Vilevile
ameongeza kwa kusema wasigeuze uimbaji kama biashara kwasababu waimbaji wana nafasi kubwa ya
kuwavuta watu kutoka kwa shetani kuja kwa Yesu na kama waimbaji wakizingatia
hilo na Mungu atanafungulia baraka juu yao.
Pia
Bw.Gembe amemaliza kwa kusema mbali na kumtangaza kristo kwaya yao wameamua
kuwa wajasiliamali kwa kuzalisha bidhaa kama Sabuni za kufuria, Dawa za chooni pamoja na Pilipili ambazo huwasaidia waimbaji
wasio kuwa na ajira kuziuza bidhaa hizo na kupata pesa za kujikimu kimaisha
jina la kampuni ni “SHUJAA MWENYE NGUVU”
Kujipatia
bidhaa hizo za “SHUJAA MWENYE NGUVU”
Piga simu namba : +255 717 461 193
Kwa picha zaidi za bidhaa zinazo zalishwa na kampuni ya shujaa mwenye nguvu






0 Maoni