MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar
es Salaam imemuhukumu Msanii wa Filamu, Elizabeth Micheal (Lulu) kutumikia
kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila
kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba, anaandika Faki Sosi.
Hukumu iliyosomwa na
Jaji Sam Rumanyika imemtia hatiani Lulu kuwa alimuua msani mwenzake, Marehemu
Kanumba bila kukusudia usiku wa Aprili 7, 2012 Sinza Kinondoni Dar es Salaam.
Kwa mara ya kwanza
Lulu alifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 12, 2017, lakini
baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
chini ya Jaji Rumanyika aliyesoma hukumu hiyo leo.
Jaji Rumanyika anesema
amemtia hatiani lulu kuuwa bila kukusudia kwa kuzingatia kifungu cha 195 cha
sheria.
Upande wa Jamhuri
ulileta mahakamani mashahidi wanne wakiwemo Seth Bosco ambaye ni mdogo wake
Marehemu Kanumba, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba moja na marehemu na
aliyekuwepo siku ya tukio, Dk. Paplas Kagaiga aliyekuwa Daktari wa familia hiyo
ambaye aliyefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba mara baada ya kudondoka.
Wengine ni Daktari
kutoka kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyeufanyia uchunguzi mwili wa
Marehemu Kanumba pamoja askari ASP Ester aliyefanya upelelezi kwenye tukio hilo
pamoja na kumtia mbaroni Lulu.
Lulu aambaye anatetewa
na wakili Peter Kibatala, waliwasilisha mashahidi wa wawili ambao ni Lulu
mwenyewe aliyehadithia mazingira ya tukio na kueleza kuwa hakuhusika kwa namna
yoyote kwenye kifo cha Marehemu Kanumba.
Wakili wa Lulu,
Kibatala amesema wanajipanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
SOURCE. MWANAHARISI ONLINE


0 Maoni