NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Muimbaji
na mwandishi wa mashairi ya nyimbo za
injili Tanzania Bw. Heri Mboya ameeleza sababu zinazo sababisha waimbaji wa
nyimbo za injili Tanzania kuja kwa kasi wanapoanza huduma hiyo na kupotea kwa
muda mfupi na wengine kupotea moja kwa moja katika huduma hiyo ya kumtumikia
Mungu kwa njia ya uimbaji.
Aidha
Bw. Mboya ameieleza plan media kuwa wengi wao hupoteza ladha ya muziki wa injili
na kuiga miziki ya kidunia “Tabia hii inawafanya wengi wasikike kidogo tu
harafu wanapotea na mifano tunayo wazi kabisa, Miziki hii ya kidunia hasa hii
inayo itwa ya kisasa haidumu zaidi ya mwezi yaani msanii wa bongo freva anaweza
akatoa wimbo leo ndani ya mwezi huohuo wimbo unachuja. Sasa muimbaji wa nyimbo
za injili kama nae akiiga huko unataka
tutegemee nini kama si kupotea ndani ya muda mfupi?”
Vilevile
Bw. Mboya amesema kwamba waimbaji wengi ni wasanii na siyo waimbaji hivyo mtu
ambae ni msanii hata utunzi wake wa mashairi ya nyimbo huwa hawamshirikishi Roho mtakatifu na badala yake wanatumia akili
na ujanja wao hivyo wimbo wainjili kama hauna uvuvio wa Roho mtakatifu hauwezi
kudumu.
Mboya
ameleza kuwa hivi sasa kuna ushindani mkubwa kwasababu waimbaji ni wengi sana
hivyo ili muimbaji aweze kuendelea vizuri ni lazima awe anamshirikisha Mungu katka kila afanyalo ili
aweze kumsaidia awe na nyimbo nzuri, waimbaji wengi hawasomi neono la Mungu kwa
wingi hili husababisha kuimba nyimbo ambazo hazina ubora zinazo sababisha
waimbaji hao kupotea.
Pia
amesema kuwa sababu nyingine ni matangazo ya muziki huo kuwa changamoto kwa
waimbaji hivyo waimbaji hasa chipukizi wanashindwa kumudu gharama za kuutangaza
muziki wao kupitia vyombo mbalimbali vya
habari ikizingatiwa kuimbaji hao wanashindwa
kulipa gharama hiyo hivyo hilinalo linasababisha waimbaji wachanga kuja na
kupotea.
Vilevile
Mboya amesama kuwa kiburi,Ujeuri, Majivuno pamoja na kutangatanga hii huwapoteza waimbaji
wengi kwasababu baadhi yao wakisha inuka na kuwa na majina wanainua mabega na
kusahau kuwa alie wapandisha ni Mungu, hii humchukiza Mungu hivyo Mungu
huwashusha na wanapotea kabisa masikioni mwa watu.
Hata
hivyo Mboya ametoa ushauri kwa waimbaji wa nyimbo za ijili Tanzania, Mboya amesema
waimbaji wapendane na hii ni kwa wakongwe pamoja na wanao chipukia kwasababu neno la Mungu linasema “Amri kuu
tuliyopewa ni upendo” lakini kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania bado neono hilo halitiliwi maanani “Mungu atusaidie”
Vilevile
amewasa waimbaji wawe rohoni na wasiimbe kwa
ajiri ya kuwaburudisha watu pekee hivyo wakumbuke dhima ya nyimbo za
injili ni kumtumikia Mungu , Kumsifu na kumuabudu katika Roho na kweli.
Pia
Bw. Mboya anawakaribisha kwenye tamasha la uzinduzi wa albamu yake inayoenda kwa jina la “ANAJIBU MAOMBI”
Tarehe 25/11/2017 ni siku ya jumamosi kuanzia saa 1:00 mchana kanisa la [E.A.G.T] Viwanja vya Mbugani Mbozi mkoani Songwe, Albamu hii iko katika
mfumo wa [DvD/VIDEO] Hivyo usikose kununua albamu hiyo ikiwa na nyimbo zenye
upako. Kutakua na waimbaji kutoka
sehemu mbali mbali na kutoka Dar es salaam atakuwepo Emanuel Mbasha pamoja na
Matumaini.
Wasiiana
na Heri Mboya kwa:
Namba; 0655 174 178
Facebook
: Heri Mboya


0 Maoni